
Watu wengi huonekana wazima kwa macho, lakini kwa ndani miili yao huwa inaathiriwa na madhara ya vyakula tunavyokula kila siku. Mara nyingi mtu huishi bila kujua kuwa ana tatizo la kiafya linaloendelea kimya kimya. Ndiyo maana ni muhimu kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara katika vituo vya afya ili kugundua magonjwa mapema, ikiwemo ugonjwa wa kisukari.
Ugonjwa wa kisukari unapogunduliwa mapema, unaweza kudhibitiwa kwa urahisi na kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea baadaye. Hizi hapa ni baadhi ya dalili za awali ambazo mtu mtarajiwa wa ugonjwa wa kisukari anaweza kuzionyesha:
1. Kupata Njaa za Mara kwa Mara
Mtu huhisi njaa kali mara kwa mara hata baada ya kula chakula. Anaweza kula, lakini baada ya muda mfupi akajikuta anahisi njaa tena bila sababu ya wazi.
2. Kuongezeka kwa Uzito kwa Kasi
Kutokana na kula mara kwa mara, mtarajiwa wa kisukari anaweza kuongezeka uzito haraka, hali ambayo huwa vigumu sana kuipunguza licha ya juhudi za kufanya mazoezi au kupunguza chakula.
3. Kupungua kwa Hamu ya Tendo la Ndoa
Mtu anaweza kukosa kabisa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Wengine hupata maumivu katika sehemu za siri au kushindwa kabisa kushiriki tendo hilo ipasavyo.
4. Changamoto za Uzazi (Ugumba)
Kwa wanawake, ugonjwa wa kisukari unaweza kuathiri mfumo wa uzazi na kusababisha kushindwa kupata ujauzito, mimba kutoka mara kwa mara, au ugumu wa kubeba mimba mpaka mwisho.
5. Weusi Kwenye Mikunjo ya Ngozi
Mtarajiwa wa kisukari anaweza kupata mabadiliko ya rangi ya ngozi, hasa katika maeneo yenye mikunjo kama shingoni, kwapani, mapajani au chini ya matiti. Weusi huu hauondoki hata kwa kutumia vipodozi.
6. Uchovu Mkali wa Mwili
Mtu huhisi uchovu wa kudumu, hata bila kufanya kazi nzito. Uchovu huu mara nyingi huambatana na dalili zinazofanana na malaria, hali inayomfanya mtu ashindwe kufanya shughuli zake za kila siku kwa ufanisi.
Nakushauri kupata Kitabu cha 𝗦𝗮𝘆𝗮𝗻𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗠𝗮𝗽𝗶𝘀𝗵𝗶. Kitabu kinatoa elimu ya manunuzi, elimu ya magonjwa ya lishe, elimu ya vyakula sahihi kwa afya na mpangilio wa chakula utakaokusaidia kuondokana na magonjwa ya lishe kama kisukari, kitambi na uzito mkubwa, shinikiizo la damu upungufu wa nguvu za kiume n.k.
KWA USHAURI NA MATIBABU
Karibu 𝗡𝘀𝗮𝗺𝗯𝗼 𝗛𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵𝗰𝗮𝗿𝗲 tupo mkabala na 𝗵𝗼𝘀𝗽𝗶𝘁𝗮𝗹𝗶 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝘆𝗮𝗺𝗮𝗹𝗮.
Tupigie 𝟬𝟳𝟲𝟳𝟬𝟯𝟬𝟭𝟲𝟬

