𝐓𝐎𝐅𝐀𝐔𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐍𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐍𝐘𝐄𝐊𝐔𝐍𝐃𝐔 𝐍𝐀 𝐍𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐍𝐘𝐄𝐔𝐏𝐄

different types raw meat beef 260nw 2233247387 e1718956613939

Nyama nyekundu ni nyama ambayo inapatikana zaidi kwa wanyama wenye jamii ya miguu minne kama vile mbuzi, kondoo, ng’ombe n.k

 𝑱𝑬, 𝑲𝑾𝑨𝑵𝑰𝑵𝑰 𝑰𝑵𝑨𝑰𝑻𝑾𝑨 𝑵𝒀𝑨𝑴𝑨 𝑵𝒀𝑬𝑲𝑼𝑵𝑫𝑼?

Kinachosababisha kuitwa nyama nyekundu ni kwasababu misuli ya wanyama hao wenye miguu minne  inatokana na misuli yao kuwa na wingi wa kiini chekundu kinachoitwa Mayoglobin.

Hiki ni kiini chekundu ambacho huwa kinapatikana katika misuli ya wanyama na kazi yake ni kunasa oksijeni inayohitajika wakati wa kuzalisha nishati mwilini. Wingi wa mayoglobin katika misuli ndivyo inavyoweza kuwasaidia wanyama hao waweze kuhimili shuhuli zao za mwili kama kutembea, kusimama n.k

 𝑱𝑬, 𝑾𝑬𝑲𝑼𝑵𝑫𝑼 𝑾𝑨 𝑵𝒀𝑨𝑴𝑨 𝑵𝑫𝑰𝑶 𝑼𝑩𝑨𝒀𝑨 𝑾𝑨 𝑵𝒀𝑨𝑴𝑨?

wekundu wa nyama sio ubaya wa nyama kwasababu nyama kuwa nyekundu kunasababishwa na wingi wa kiini cha mayogblin ambacho kinasaidia kutengeneza nishati ili mnyama aweze kufanya shuhuli zake anazofanya kama kutembea, kusimama. Ni sawa na majani kuwa na rangi ya kijani kwasababu ya kijani kiwiti ambacho kipo ndani ya jani la mmea inayosaidia mmea kujipatia chakula chake.

𝐍𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐍𝐘𝐄𝐔𝐏𝐄

Nyama nyeupe inatokana na wanyama na ndege kama samaki, kuku, bata, kware, kanga n.k.

Weupe wa nyama ni kwasababu ya kuwa na kiwaago kidogo cha mayoglobin, kwa mfano nyama ya samanki, kuku n.k wanakiwango kidogo cha mayoglobin ndio maana nyama zao ni nyeupe.

𝑱𝑬 𝑴𝑻𝑼 𝑨𝑲𝑰𝑳𝑨 𝑵𝒀𝑨𝑴𝑨 𝑵𝒀𝑬𝑼𝑷𝑬 𝑨𝑵𝑨𝑷𝑨𝑻𝑨 𝑭𝑨𝑰𝑫𝑨 𝒁𝑨𝑰𝑫𝑰 𝑲𝑰𝑨𝑭𝒀𝑨 𝑲𝑼𝑳𝑰𝑲𝑶 𝑨𝑵𝑨𝑬𝑲𝑼𝑳𝑨 𝑵𝒀𝑨𝑴𝑨 𝑵𝒀𝑬𝑲𝑼𝑵𝑫𝑼?

Wekundu wa nyama sio ubaya wa nyama na weupe wa nyama sio uzuri wa nyama.

Hakuna tafiti iliyowahi kufanyika na kusema kwamba mayoglobin iliyopo katika nyama nyekundu inaleta maradhi ya lishe.

Nyama nyekundu ilisemekana kuwa ni mbaya kutokana na nadharia mbalimbali zinazosema kwamba mafuta yanayoganda yanaleta magonjwa ya moyo ndio mana nadharia hii ikafanikiwa kuigandamiza nyama nyekundu na kuonekana mbaya.

Kwa upande wa nyama nyeupe ilionekana nzuri kwasababu ina kiwango kidogo cha mafuta yanayoganda na kuonekana kuwa ni nyama nzuri. Nadharia ya mafuta ndio inayofanya kuhama kutoka kwenye nyama nyekundu na kuhamia kwenye nyama nyeupe.

Kitendo hiko kimesababisha kuibuka kwa kuku wa kisasa, samaki wa kufugwa kwenye mabwawa wanaoweza kuzaliana kwa kasi kwasababu ya kutimiza uhitaji mkubwa wa nyama nyeupe kwa watu.

Kutokana na nadharia hizo na elimu  kuhusu nyama nyeupe na nyama nyekundu ndio iliyosababisha kutengenezewa kwa nyama za maabara badala ya kula nyama asilia.

Katika kutekeleza Sayansi ya Mapishi huwa hatushauri mtu kula kuku wa kisasa kwasababu kuku wa kisasa wanalishwa mashudu na nafaka lakini pia wanawekewa homoni tofauti na kuku anayejichunga mwenyewe.

Mashudu na nafaka wanazokula kuku wa kisasa yana mafuta mengi ya Omega 6 ambayo yakijaa mwilini yanasababisha pumu ya ngozi, kifua, shinikizo la damu, shambulio la moyo au shambulio la ubongo n.k

Kwahiyo kama unataka kula nyama nyeupe ni bora kula kuku wa kienyeji ambaye hana hatari ya kiwango cha sindano na kemikali bali anajichunga mwenyewe na kula vyakula asilia.

Kati ya nyama ya kuku wa kisasa na nyama ya ngombe, ni bora kuchagua nyama ya ngombe ambayo ni bora kutokana na wingi wa mafuta ya Omega 3 kutokana na vyakula anavyokula ikiwemo nyasi asilia tofauti na nyama ya kuku ambayo imejaa vihatarishi vinavyoweza kusababisha magonjwa ya moyo na magonjwa mengine.

Kwahiyo nyama ya n’gombe sio mbaya bali ni nyama bora kuzidi nyama ya kuku hata wale wa kienyeji.

𝑴𝒂𝒎𝒃𝒐 𝒚𝒂𝒏𝒂𝒚𝒐𝒇𝒂𝒏𝒚𝒂 𝒏𝒚𝒂𝒎𝒂 𝒏𝒚𝒆𝒌𝒖𝒏𝒅𝒖 𝒌𝒖𝒐𝒏𝒆𝒌𝒂𝒏𝒂 𝒎𝒃𝒂𝒚𝒂:

 𝗞𝘂𝗹𝗮 𝗻𝘆𝗮𝗺𝗮 𝗶𝗹𝗶𝘆𝗼𝘀𝗶𝗻𝗱𝗶𝗸𝘄𝗮 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝗮𝗸𝗼𝗽𝗼.

Nyama hizi huwa zinawekwa kemikali ambazo zinazuia nyama isipoteze ukali wake, kemikali hizo zinapochomwa kwenye mafuta hutengeneza sumu zinazoweza kukuletea magonjwa kama kansa.

 𝗞𝘂𝗸𝗮𝗮𝗻𝗴𝗮 𝗻𝘆𝗮𝗺𝗮 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝗮𝗳𝘂𝘁𝗮 𝘆𝗮𝘀𝗶𝘆𝗼𝗵𝗶𝗺𝗶𝗹𝗶 𝗺𝗼𝘁𝗼.

Kitendo cha kuchukua nyama ambayo haina mafuta na kuichoma au kuikaanga kwenye mafuta ambayo hayahimili moto kama mafuta ya pamba, mahindi, alizeti au soya.

Mafuta hayo yanapoungua huwa yanatengeneza sumu nyingi 𝑭𝒓𝒆𝒆 𝒓𝒂𝒅𝒊𝒄𝒂𝒍𝒔 ambazo zinapenya na kuingia kwenye nyama, unapokula nyama hiyo unakula na hizo sumu ambazo zikijaa mwilini zitasababisha uvimbe kwenye kizazi, pumu ya ngozi pumu ya kifua, na magonjwa sugu zaidi.

 𝗞𝘂𝗮𝗺𝗯𝗮𝘁𝗮𝗻𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗻𝘆𝗮𝗺𝗮 𝗻𝗮 𝘃𝗶𝗻𝘆𝘄𝗮𝗷𝗶 𝘃𝘆𝗮 𝘀𝘂𝗸𝗮𝗿𝗶 𝗮𝘂 𝗽𝗼𝗺𝗯𝗲.

Kitendo cha kupitisha nyama kwenye mafuta mabaya na kuambatanisha na kinywaji chenye sukari kama vile soda, juisi au pombe kitaumiza mwili wako kwasababu mwili ukipokea chakula cha mafuta na sukari huanza kutumia sukari kwanza na kile cha mafuta kinaachwa hakitumiki. Hali hiyo inaweza kukufanya upate uzito kupindukia na magonjwa mbalimbali.

𝑴𝒂𝒎𝒃𝒐 𝒚𝒂 𝒌𝒖𝒛𝒊𝒏𝒈𝒂𝒕𝒊𝒂 𝒘𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊 𝒘𝒂 𝒌𝒖𝒄𝒉𝒂𝒈𝒖𝒂 𝒏𝒚𝒂𝒎𝒂 𝒏𝒚𝒆𝒌𝒖𝒏𝒅𝒖 𝒂𝒖 𝒏𝒚𝒂𝒎𝒂 𝒏𝒚𝒆𝒖𝒑𝒆.

Kabla ya kutaka kuchagua nyama nyekundu au nyama nyeupe, inatakiwa kuondoa mafikirio ya kwamba nyama nyeupe ni nzuri kiafya na nyama nyekundu ni mbaya kiafya. Nyama yenye ubora ni nyama ya samaki, nyama ya wanyama wenye miguu minne pamoja na nyama ya kuku.

Unapokula nyama zingatia kula na mafuta yatokanayo na nyama hiyo kwasababu mafuta asili yanayotoka kwenye nyama ni tiba, huku ukiambatanisha na mboga za majani, karanga za almond, korosho n.k

Sayansi ya mapishi inatushauri sana kula nyama asilia ambayo imetoka buchani au umeiandaa mwenyewe kama vile kuchinja kuku wa kienyeji, inashauri kujiepusha ulaji wa nyama zinazotokana na kemikali, ili kujikinga na magonjwa mbalimbali.

Jifunze zaidi; tazama video hii:

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *