Ushawahi Kusikia Ukitaka kuwa na afya njema kuwa VEGAN yaani Mtu anayekula Vyakula vinavyotokana na Mimea tu yani, hali nyama kabisa.
Vegan ni taasisi yenye watu wachache tu duniani ila ina nguvu sana. Taasisi hii ilifanikiwa hadi sera zake za Lishe kuingizwa katika miongozo ya ushauri.
Ushawahi kusikia mtu anakwambia βMimi sili Nyama Samaki Kuku mayai? Nakula nafaka, Mizizi,mboga za majani na matunda tu? β Hawa tunao lakini bado βHuwa nakutana nao clinic wana Kitambi, Kisukari,Shinikizo la damu, Magonjwa ya mifupa nk.
Huwa natafakari bila jibu kamili, hivi inakuwaje unaishi kwa Kuepuka vyakula vya wanyama lakini bado unakabiliwa na magonjwa sugu na hustuki yawezakuwa sio njia sahihi ya kula kiafya?
Kuna siku moja nilikutana na βMgonjwa mmoja kisukari kimemchakaza sana, Nikamshauri Ale kuzingatia kanuni zangu za @sayansiyamapishi . Akasema βSiwezi Kuacha wali maharage naupenda sanaβ Ila pia sili vitu vyote vya wanyama. Na kila mara anazidiwa na kupelekwa India kwa sababu ya sukari Kupanda.

SIO SAHIHI KUTOKULA VYAKULA VYA WANYAMA
1. Binadamu mfumo wake wa Chakula haufanani na Mfumo wa Mifugo inayokula nyasi. Binadamu hawezi kusaga Mimea kwa wepesi kama Mifugo ambayo hadi Hucheua ili kukisaga zaidi.
Sisi sio wamajaniβ¦
2. Ukitazama kinywa cha binadamu kuna meno yaliyo chongoka pembeni huitwa Canine Teeth kazi yake ni βKukata kitu kigumu kama nyamaβ na sio Ugali wali ndizi Juisi tambi nk.
3. Enzi za kale nafaka tulikula kwa uchache sababu tulikuwa na nyenzo duni za kilimo na nyenzo duni za kusindika mahindi mtama na ngano kuwa unga. Tulitumia mawe kusaga. Huwezi lisha familia. Chakula kikuu kilitokana na βuwindaji,Ufugaji na Uvuviβ
5. Ukisikia βSuperfoodsβ au βNutrient dense foodsβ yaani vyakula vyenye Virutubisho vingi ni βNyama,samaki,kuku,mayaiβ na sio Wali,Ugali,ndizi,viazi tambi nk
6. Wagonjwa wangu wengi hupona kwa kuwaachisha vyakula visivyo na virutubisho na kuwaambia wale 75% vyenye virutubisho miezi 4-6 huku nikiwaongezea walivyo pungukiwa kwa miaka yote waliokula bila kujua. Muda wa siku 120 hunisimulia ushuhuda mkubwa sana ktk mwili.
7. Vegan anakwambia Asilimia 55-60 ya unachokula kiwe ni βWanga na sukariβ na asilimia inayofuata ni Protini halafu mafuta hupigwa vita sana. Hivyo chakula chake kinakuwa ASILIMIA KUBWA KINA UHABA WA VIRUTUBISHO AKILA HIVYO MIAKA LAZIMA AFYA YAKE IKONGOROKE.
8. Usipokula vyakula vya wanyama lazima kila siku iendayo kwa Mungu ule Virutubisho katika mfumo wa Kidonge la sivyo utaugua upungufu wa hivyo virutubisho. Mfano Vitamin A, D, E ,K , Omega 3, na Vitamin B12. Makopo ya hizi dawa ni bei kubwa sana Huwezi kutumia Milele.
βNjia rahisi ni kubadilisha muundo wa sahani ili virutubisho hivyo Uvipate kwenye Sahani ya chakula unachokula kila sikuβ
9. Kuwa Vegan hakumfai kila mtu. Ndio maana kuna watu ni vegan ila wana Kitambi, Kisukari nk. Sasa Inakuwaje anapata kitambi wakati hanywi Pombe, Hali vyakula vya mafuta? Hapa ni Adui yupo kwenye sahani yake.
Kiufupi tu βKama unavyoishi unazidi kunenepa na kuumwa basi mwili wako haukustahili kula jinsi unavyokulaβ

UNAWEZA JIUNGA NA MASOMO YANGU KWA KUTUMA UJUMBE KWENYE INBOX βLISHE BORA 2026β
SHARE WATU WAPONE NAOMBA NIPATE SHARES 100 LEO NITASHUSHA MAKALA NYINGINE NZITO


