𝗨𝗣𝗨𝗡𝗚𝗨𝗙𝗨 𝗪𝗔 𝗩𝗜𝗧𝗔𝗠𝗜𝗡 𝗗, 𝗦𝗔𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗨𝗠𝗜𝗩𝗨 𝗬𝗔 𝗠𝗜𝗙𝗨𝗣𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗜𝗙𝗨𝗣𝗔 𝗞𝗨𝗣𝗔𝗦𝗨𝗔.

different types raw meat beef 260nw 2233247387 e1718956613939

𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 ni vitamin ambavyo huwa inatembea na vyakula vyenye mafuta na lehemu (cholesterol). Endapo usipokula vyakula vyenye mafuta basi mfumo wako wa chakula utakuwa na upungufu wa 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫.

Ukichukua mayai ukatupa kiini cha njano utakuwa umetupa𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 kwasababu vipo kwenye kiini cha yai, hata ukichukua maziwa ukamwaga yale mafuta ya juu utakua umemwaga 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 kwasababu ipo kwenye yale mafuta ya juu .

Endapo mtu asipokula samaki, nyama atakua anapungukiwa 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫, kwahiyo 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 inapatikana kwenye vyakula vyenye mafuta, lakini  vyakula ambavyo havina mafuta vinauhaba wa 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫, ndio maana wataalam wanasema 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 ni vyakula vya mafuta yaani Fat soluble vitamin.

Watu wengi wanahangaika na maumivu makali ya mifupa huwa wanapungukiwa na aina hii ya vitamini ambayo inapatikana kwenye vyakula vya mafuta kwa wingi.

Mambo yanayoweza kusababisha kupungukiwa 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 ni pamoja na ;

📌𝐊𝐮𝐰𝐚 na u𝐳𝐢𝐭𝐨 𝐦𝐤𝐮𝐛𝐰𝐚 𝐚𝐮 𝐮𝐧𝐞𝐧𝐞 𝐮𝐥𝐢𝐨𝐤𝐢𝐭𝐡𝐢𝐫𝐢。

Kadiri mtu anavyozidi kubeba uzito mkubwa ndivyo mifupa yake inavyoongezeka kudhoofika kwa haraka sana kutokana na uzito uliopitiliza.

📌 𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗿𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗳𝗶𝗴𝗼.

Ili uweze kupata 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 kama vile kukaa kwenye jua haiwezi kusaidia kama unasumbuliwa na magonjwa ya figo. Kwahiyo unahitajika kuwa na figo yenye afya ili iweze kuimarisha afya ya mifupa yako. Itakua kazi sana kupata 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 hata kwa kumeza vidonge kwasababu vidonge vya 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 vinatakiwa kufanyiwa kazi kwenye figo ili viweze kuimarisha mifupa.

📌𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗶𝗻𝗶.

𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 inayotengenezwa kutoka kwenye ngozi baada ya kupigwa na mwanga wa jua haiwezi kufanya kazi yake kuimarisha mifupa kama ini linamatatizo ndio mana tunasisitiziwa kulinda ini na figo ili kuimarisha mifupa mpaka uzeeni.

Kwahiyo unaweza kutumia dawa au supplement mbalimbali za 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 kwa lengo la kuimarisha mifupa yako lakini usipate manufaa kwasababu figo na ini zinamatatizo, kwahiyo unatakiwa kupata njia ambayo itakusaidia katika tatizo lako.

katika mwili wa binadamu kuna seli zinazojenga mifupa na katika mifupa kuna seli zinazobomoa mifupa. 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 ikiwepo ya kutosha mwilini huzifanya seli zinazojenga mifupa ziweze kufanya kazi kwa hali ya juu na kuimarisha mifupa yako.

Endapo 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 ikipungua katika damu na kutokuwepo ya kutosha, mwilini hapo ndipok utakapoanza kupata maumivu makali sana ya mifupa, mifupa kupasua n.k

Kama chakula ulichokua unakila kilikua na shehena kubwa ya vyakula vya wanga na vinywaji vyenye sukari tupu ambavyo havina utajiri wa 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 itabidi uache na uanze kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 kama vile mayai na kiini chake, kula samaki, kunywa maziwa na mafuta yake, kula karanga zenye mafuta mengi ya omega 3 na𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 kwa wingi kama almonds au korosho, kweme na mbegu za maboga n.k

Kitu cha kwanza ni kuutajirisha mwili kupata vyakula vyenye shehena kubwa ya𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫, lakini pia kupata virutubisho vya 𝑽𝒊𝒕𝒂𝒎𝒊𝒏 𝑫 ambavyo vitakusaidia kuimarisha afya ya mifupa yako.

Jifunze zaidi; Tazama Video hii 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *