𝐒𝐀𝐁𝐀𝐁𝐔 𝐙𝐀 𝐕𝐈𝐃𝐎𝐍𝐃𝐀 𝐕𝐘𝐀 𝐓𝐔𝐌𝐁𝐎

vidonda vya tumbo 768x432 (1)

Nuru ya macho imekuwa ni kilio cha wengi sana katika nyakati za sasa. Watalamu wamekuwa wakihusisha ongezeko hili na mlipuko wa ugonjwa wa kisukari, na kusemekana ni athari za ugonjwa huo. Lakini pia wengi wamekuwa wakihofiwa kuwa lishe yao haihusishi vyakula vyenye vitamin A kwa wingi na hivyo hushauriwa kutumia vyakula vyenye vitamin A kwa wingi.

Ushauri ulio zoeleka kwa wagonjwa wengi wenye matatizo kama haya hapa Tanzania, ni watalamu kuwashauri wagonjwa kutumia juisi ya tembele,karoti na kitunguu pori (beet roots) kwamba vinasaidia kuwapatia vitamin A kwa wingi. Bila kusahau wanashauriwa kula aina mbalimbali za matunda na mboga za majani, wengi wao hutumia njia ya utengenezaji wa juisi za matunda ili wajipatie vitamin hizo kwa wingi wakisimamia mgongo wa kwamba wanakunywa kinywaji ambacho kina sukari asili na wanalenga kurudisha nuru ya macho na afya ya mwili kiujumla.

Lakini mbali na kufanya hivyo, njia hizo hizo zimebaki kitendawili kuwarudishia nuru ya macho na hata kupata nafuu ile ndogo hawapati tofauti na afya ya mwili kuendelea kudhoofika kila kukicha. Hebu leo tutajaribu kuangalia mambo mbalimbali ambayo hata mtalamu wako yawezakuwa hajawahi kukuambia na inaweza kuwa ndio sababu hupati nafuu ya kiafya. Kumbuka elimu ya sayansi ya mapishi kwa takribani miaka Zaidi ya 4 imekuwa ikitoa elimu kwa jamii kwa kushughulikia mzizi au chanzo cha tatizo na sio kuhangaika na dalili wakati chanzo chenyewe kiuhalisia hujagundua.

stomach infographic 1308 39675

Unapokosa nuru ya macho yawezakuwa mambo mbalimbali yamekusibu kiafya hivyo natoa ushauri kwanza, kama unasumbuliwa na matatizo ya macho mwone daktari wa macho akupime kwa kina na atakushauri vizuri kulingana na vipimo na dawa unazotakiwa kutumia maana visababishi ni vingi ikiwemo kuharibiwa kwa miundo mbinu ya mishipa ya damu ya macho hasa wagonjwa wa kisukari, mtoto wa jicho,Uvimbe kwenye ubongo,Shinikizo la damu,Maambukizi ya muda mfupi ya bakteria,Upungufu wa vitamin A  nk. Pata kwanza vipimo itakusaidia wewe kujua upo kundi gani na ushauri utakusaidia sana.

Leo mimi nitakusia jinsi ambavyo mwili wako unaweza kupungukiwa vitamin A na namna ya kuboresha hili tatizo maana lipo chini ya mamlaka yetu maana vitamin A chanzo chake kikuu ni chakula,ina maana tiba sote tunayo ni jukumu letu kujua namna ya kuitumia.

Lakini pia nimehusisha Upungufu wa vitamin A na ulaji wa vyakula vya wanga na sukari unaweza kujiuliza kwa nini? Ni kwamba,Unapokula chakula unatarajia kwamba upate manufaa kutoka kwenye chakula hicho kama vitamin,madini,nguvu na joto. Ila sasa yote hayo utayapata kwa ufanisi mkubwa endapo mfumo wa chakula utakuwa una afya njema. Narudia tena haya maneno “Endapo mfumo wa chakula utakuwa una afya njema”kwa maana yake kama mfumo wa chakula ni mbovu hata ufanisi wa kukupatia kile unacholenga kwenye chakula unachokula hutaweza kukipata utakuwa ni upotevu wa pesa na muda. Hata kama ukinywa galoni 5 kila siku za juisi ya karoti, juisi ya tembele na juisi za matunda mengine kwa lengo la kupata vitamin A hutaweza kupata unacho dhamiria kama mfumo wa chakula hauna afya njema.

Je ni lini mshauri wako amekaa na wewe kuchunguza kwa kina kama mwenendo wako unaimarisha mfumo wa chakula au unabomoa mfumo wa chakula? Kama hakuna hata mmoja kwa nini unakata tamaa kuendelea kutafuta maarifa? Upungufu wa maarifa ya afya katika jamii ni ugonjwa unao tafuna maelfu ya watu na kuwapotea pesa nyingi na kuharibu uchumi wa familia n ahata kupoteza matumaini ya kuishi duniani.

Mnamo mwaka 2010 kwa mara ya kwanza mwanasayansi na mtafiti Inna Sekirov na wenzake 3 alitoa tafiti iliyo onesha “Uhusiano wa afya ya mwili wako na mfumo wa chakula” (INNA SEKIROV 2010) moja ya maneno ya ripoti yao yaliyobeba karibia ujumbe wote ni haya mawili “death sits in the bowels” and “bad digestion is the root of all evil”. Yaani chanzo cha kifo ni ndani ya mfumo wa chakula, na Mfumo mbovu wa mmengényo wa chakula ni chanzo cha maafa yote kiafya. Ulimwengu ulitingishika na walionesha kwamba katika mfumo wa chakula huwa kuna vimelea au bakteria rafiki ambao wanakadiliwa kuwa ni mara ya kumi ya seli zinazo tengeneza mwili wako (rudia hio sentensi) ina maana sasa endapo ukiwatengenezea mazingira mabaya hao bakteria rafiki wanaokulinda,wanaokuwezesha uwe mwenye afya njema basi wanakufa na bakteria wabaya wanaanza kushambulia mfumo wa chakula hatimaye mmengényo wa chakula unaharibika na ufanisi wa mfumo wa chakula nao unaharibika.

gastric acid royalty free image 1619717510 600x600

Sio wanasayansi hao tu, mwaka 2011 Mwanasayansi alijaribu kuonesha  kwa kina kwa nini wale bakteria rafiki wanapo uwawa kwa lishe mbovu na mifumo mingine mfano unywaji pombe kupindukia, wanasababisha bakteria maadui kuzaliana kwa wingi,na kudhoofisha mfumo wa chakula. Ninaposema kudhoofika maana yake mfumo wa chakula unakuwa haumengényi vizuri chakula kila unapokula kunaambatana na gesi na kiungulia sana na kuharisha au tumbo kusokota kama vile una homa ya tumbo,Chakula ambacho hakijamngénywa vizuri kinafanikiwa kupenya kuingia kwenye damu wakati kawaida huwa haviruhusiwi, hali hio huirwa kitalamu “Leaky Gut”yaani mfumo wa chakula unaanza kupenyeza kitu ambacho hakiruhusiwi kupenya kama chakula ambacho hakijawa kamili,bacteria nk. Sasa wanasayansi hawa walionesha jinsi hao bakteria wabaya wanavyo fanya mfumo wako upate hitilafu yaani “Leaky Gut”itokee. Tafiti yake ilipewa jina la (ALESSIO FASANO 2011). Mwanasayansi huyu Allesio Fassano anajulikana sasa kama muasisi wa “Leaky gut”kwani maisha yake amewekeza kuonesha uhusiano kati ya magonjwa ya mashambulizi ya mwili kama magonjwa ya pumu ya kifua,pumu ya ngozi,SLE, Magoti na viungo vingine jinsi gani yana uhusiano na afya ya mfumo wa chakula.

Sambamba na tafiti hio mwaka uliofuata Allesio Fassano alitoa tena tafiti yake ikionesha namna ya kugundua maradhi ya mfumo wa chakula jinsi gani yana uhusiano na mashambulizi ya mwili (Allessio Fassano 2012). Katika chapisho hilo magonjwa hatari ya mfumo wa chakula kama Crohn’s disease na IBD (Irritable Bowel disease) magonjwa haya yote ni tishio katika mfumo wa chakula yana ambatana na dalili kama Choo kigumu sana, Kutokwa damu kwenye haja kubwa, Kupungukiwa damu kwa muda mrefu, gesi, tumbo kuuma sana hasa unapokula tu linaanza kuvuruga nk. Kuna uhusiano mkubwa kati ya Magonjwa haya na upungufu wa vitamin A na viini lishe vingine.

Lakini kuna tafiti  na machapisho sasa Zaidi ya 3517 nilipojaribu kutafuta kwenye tovuti ya  US national Libriary of Medicine (NIH) kwa kuandika neon “Leaky Gut”hapa nataka kusema kwamba kuna tafiti za kutosha kuhusu hiki ambacho nakihusisha hapa na nimekuwa nikiwashauri wanafunzi wangu wa sayansi ya mapishi kuishi kwa kulinda mfumo wa chakula ingawaje katika mfumo wa tiba ya kawaida bado magonjwa haya ya mfumo wa chakula kama IBS yanatibiwa kwa upasuaji pale yanapokuwa yapo hatua mbaya ingawaje lishe mbovu ina mchango mkubwa sana kama tulivyoona hapo juu.

gut health: how to protect your digestive system

Vyakula ambavyo vinatuhumiwa na tafiti zote hizo kwamba huharibu ufanisi wa mfumo wa chakula na kukuibulia magonjwa mbalimbali kimwili:

1. Sukari

Vyakula vyenye kiwango kingi cha sukari kama juisi na vinywaji vingine viwandani vya vyakula vingine vyenye mapishi yenye kuongeza sukari nyingi kama keki,mikate,vitafunwa mbalimbali. Pia kwenye vinywaji kinacho angamiza bakteria rafiki ni kiwango kingi cha sukari,kemikali inayo ongeza rangi na radha hao ni maadui wakubwa sana wa mfumo wa chakula kibaya Zaidi hujui kiwango gani wewe kikikusanyika kitakuletea madhara.

Hata hivyo hata matumizi ya juisi za kutengeneza sisi wenyewe majumbani zinaweza kuchangia wewe kupata leaky gut kwa sababu unamimina sukari nyingi kwa mkao mmoja, hata hivyo mrundikano wa mafuta kwenye Ini unadumaza ini la binadamu ambalo ni hifadhi kubwa sana ya vitamin A na matokeo yake unapungukiwa vitamin hio. Ndio maana unapozungumzia vitamin A kusa chakula mgonjwa anachokula,Pale ambapo kinaenda kufanyiwa kazi na Pale mabapo kitaenda kuhifadhiwa, Sukari inaharibu kote huko ndio maana naituhumu.

2. Vyakula vya wanga na sukari nyingi hasa ngano, wali, ugali vyakula hivi tunapokula bila kipimo yaani mapumziko vina athiri sana mfumo wa chakula. Nafaka ni adui namba mbili kuna baadhi ya watu huwa hatustahimili kwa kiwango kikubwa na mara nyingi ukiona mfumo wako wa umengényaji wa chakula unaenda ambavyo sivyo jaribu kubadilisha lishe yako utaona gesi na mengine mengi yanapotea. Ngano pia tunaituhumu kwa sababu ya kiambata ambacho wengi huwa hatuwezi kukitumia vizuri yaani gluten na ndio maana ngano sio rafiki kabisa kama unataka kurudisha mfumo wako wa chakula.

3. Mafuta yenye shehena kubwa ya omega 6 hasa mafuta yatonayo na mbegu za mimea. Haya pia sio rafiki kabisa unapotaka kurudisha kinga asili ya mfumo wa chakula yaani wale bakteria rafiki walio angamia kwa lishe mbovu. Mafuta haya ni kama alizeti,pamba,soya,margarine nk kwani yanalemaza mfumo wako wa chakula kwa kuwaua bakteria rafiki. Kinyume kabisa na mafuta mazuri yatokanayo na parachichi,nazi,ngómbe,maziwa jinsi ambavyo yanaweza kuwalea bakteria rafiki na kurudisha kinga asili ya mfumo wa chakula na afya yake ikiwemo ufanisi wake kuimarika.

4. Msongo wa mawazo wa kudumu. Hiki pia ni chanzo mojawapo wa kupata leaky gut na mfumo wako wa umengényaji kuanza kukusumbua. Mfano vichocheo vya msongo wa mawazo hufanya mfumo wa chakula kushughulikia chakula chini ya kiwango hatima yake ni gesi na kiungulia sana. Endapo ukijitahidi kujua nini hasa kinachokuletea msongo utaweza kuboresha mfumo wako wa chakula.

Haya sasa baada ya kusema hayo kumbe sasa mara baada tu ya mfumo wako wa chakula kuwa salama na wenye afya, sasa tutakuwa tumetengeneza mazingira mazuri sana ya mwili kujipatia vitamin A ambayo tumeambiwa tumepungukiwa.

Vitamin A ni jina la ukoo au jina la mjumuisho wa viini lishe aina tatu yaani retinol,retinal,Retinoic acid, kwa upamoja wake huitwa vitamin A. Vyote hivyo nilivyo taja vinapatikana kwenye vyanzo vya wanyama sio mimea hata kidogo naomba unielewe hapa. Vitamin A ambayo unaipata kwenye matembele na karoti huwa haiku tayari kwa matumizi kwa lugha nyingine huwa haipo katika mfumo huo wa aina tatu (Retinol,Retinoic acid na Retinal).

Sasa je nitapataje vitamin A kutoka kwenye matembele,karoti na mboga zingine za majani?

Jibu ni kwamba mwili huwa unajipatia vitamin A ambayo ipo tayari kwa matumizi ya mwili moja kwa moja yaani retinol, retinoic acid na retinal na vyanzo vyake vizuri ili upate hivyo viini lishe ni Maini,kiini cha yai,siagi kutoka kwenye maziwa, Maziwa menyewe nk. Kwa lugha nyingine Vitamin A huitwa kitalamu Fat soluble vitamin (Fat loving vitamin) hii ni vitamin inayo tembea popote na vyakula vya mafuta. Sio kama vitamin zingine kama Vitamin B mbalimbali,C ,Folic acid ambazo hutembea na ,maji , wagonjwa wengi wa kisukari hukojoa sana mara kwa mara hivyo hupeteza sana vitamin ambazo zinatembea na maji lakini asipokula vyakula vya mafuta salama napo atakuwa hatarini kupungukiwa vitamin aina zote (Multi vitamin deficiency).

Kwenye mboga za majani mbalimbali mwili huwa unapokea kitu ambacho huwa nakiita malighafi ya kutengeneza Vitamin A ambayo huitwa kitalamu Beta carotene. Malighafi hii ikisha ingia mwilini kwenye utumbo mwembamba hubadilishwa (Beta Carotene dioxygenase hufanya kazi hio) na kuwa vitamin A katika mfumo wa matumizi ya mwili yaani (Retinol,Retinoic acid na retinal). Kwa lugha nyingine kama mfumo wa chakula ni mbovu huwezi ukapata vitamin A kutoka kwenye mboga za majani ambazo unatumia. Yakupasa kwanza kutibu mfumo wa chakula kabla hujaendelea na hatua zingine za kurudisha vitamin A mwilini mwako.

Kwa lugha nyingine vyanzo vizuri vya vitamin A sio matembele, sio bamia,sio spinach na sio Sukuma wiki wala kabeji hata ufanisi wa mfumo wa chakula kubadilisha Beta carotene kuwa vitamin A huwa sio wa asilimia 100 kwa maana hio kama wewe huli vyakula kama mayai na kiini chake,Nyama,Maini,Maziwa nk basi yakupasa utumie vidonge ambavyo vitakurutubisha na kukupatia vitamin A. Lakini nakuonya tu kwamba kati ya vitamin zote ambazo huwa zinatembea na mafuta kama vitamin A,D E na K vitamin ambazo ukizidisha zinakuleta madhara ni vitamin A na D na sayansi inasema hivi kwa kutumia vyanzo vya vyakula vya vitamin A na D huwezi kuzidisha kiwango chake na ni virahisi sana kuanza kuuguza magonjwa ya kuzidisha vitamin A na D endapo ukitumia kwa muda mrefu na dozi ikawa kubwa kama unatumia virutibisho vidonge. Hivi kwa nini usumbuke hivyo wakati Chakula kipo ambacho kina uwezo wa kukupatia vitamin A na D kwa uwiano mzuri bila kuzidisha? Kwa nini ukanunue virutubisho wakati chakula kipo? Tumia vitu hivyo endapo tu umeandikiwa na daktari na kuna sababu ya msingi na hakuna mbadala, lakini mbadala wa vitamin A tunao, tena vyakula tu.

Hivyo basi nakushauri vyanzo vizuri vya vitamin A baada ya kuwa mfumo wako wa chakula umeutibu ni mayai, nyama, maini, siagi, maziwa, samaki, mboga za majani aina mbalimbali. Kama unapenda kula matunda kula kama yalivyo ila usikamue juisi itapendeza Zaidi ili kupunguza kitendo cha kumimina sukari nyingi kwa wakati mmoja.

vitamin a d e k 1500 900 01 50f2e6d0 3b46 49f0 879f b6dc0580c457

Ila kitu ambacho sitapenda nisahau kukufahamisha ni kwamba vitamin hizi ambazo zinatembea na mafuta ikiwemo vitamin A huwa hatuzipati kila siku kwa wingi uleule hivyo basi mwili umejengewa uwezo wa kuhifadhi vitamin A, D, E na K. Mfano Vitamin A huhifadhiwa katika Ini la binadamu ambapo Ini la binadamu lina uwezo wa kuhifadhi vitamin A kwa matumizi ya mwili yam waka mzima. Uwezo wa Ini lako kuhifadhi vitamin A ni mkubwa sana. Na Huhifadhiwa katika mfumo uitwao retinol palmitate kwa matumizi ya baadae pale ambapo kuna uhaba wake.

Hii inaleta habari mbaya sana kwa mywaji wa pombe na juisi zenye kumiminia ini la binadamu kiwango kingi cha sukari aina ya fructose. Sukari hii pamoja na pombe huleta msongo mkubwa sana kwenye Ini,huleta majeraha kwenye Ini baada ya kurundika mafuta,Huumiza Ini na majeraha hayo yanapopona huweza kutengeneza makovu ya kudumu na ndio maana unaambiwa pombe inaleta ulemavu wa Ini wa milele hata sukari aina ya fructose kutoka kwenye matunda,asali,miwa na sukari kavu tunayoweka kwenye chai matumizi ya kupindukia husababisha Ini la lenye mafuta (Non Alcoholic Fatty Liver) kama nilivyo eleza katika kitabu cha sayansi ya mapishi kwa nini mlipuko wake ni mkubwa sana na hatima yake ni Ini kufa kabisa Liver Cirrhosis. Ini lako linapofikia hatua hii lazima unakuwa hatarini sana kuwa mhangwa wa upungufu wa vitamin A kwa sababu hifadhi yake umeiharibu.

Kuna mwasayansi mmoja alifanya tafiti iliyo nukuliwa katika kitabu cha kemia ya seli ya binadamu (John W Bayness n.d.) kwamba, Mgonjwa aliyefika katika kituo cha afya akilalamika matatizo ya mfumo wa chakula na baada ya vipimo aligundulika ana IBS (rejea juu) na kutokana na hali yake waliamua kumlisha kwa mrija chakula ambacho hakikuwa na mafuta kabisa ni wanga tupu na walisitisha vidonge vya kumrutubisha vitamin A. Baada ya siku kadhaa akaanza kulalamika haoni usiku kabisa na kuja kupima kiwango cha vitamin A walikuta kipo chini sana. Daktari aliamua kufanya zoezi la pili kumpatia vyakula vyenye mafuta kama nilivyosema hapo vyenye kumpatia vitamin A, nuru yake ya macho ikarudi hata bila virutubisho vya vitamin A.

Hicho ndicho nilicho dhamiria kukufundisha leo kwamba, Kama wewe hauli vyakula ambavyo vinatokana na vyanzo vya wanyama unakula mimea pekee basi hakikisha unakuwa na virutubisho vya kukupatia kile unacho pungukiwa. Na kuwa makini sana na unapoyafanya maisha yako kwa kurutubisha vitamin A na vitamin B endapo ukila kupindukia unapata madhara kiafya tena makubwa.

Mafuta yapo mabaya na kuna mafuta mazuri, na nimetoa mfano wa vyakula vyenye mafuta salama na nimekuonesha mifano ya vyakula vya mafuta ambavyo nia adui katika mfumo wa chakula.

Kuna uhusiano mkubwa kati ya kukosa nuru ya macho kunakosababishwa na vitamin A na mfumo wa chakula kuwa hauna afya njema, Magonjwa mengi sugu na unayo ambiwa leo huwezi kupona chanzo chake ni ndani ya mfumo wa chakula, ukitaka urudishe afya yako barabarani leo pigania mfumo wa chakula urudi kwenye afya yake.

Karibu sana TUJIFUNZE NA MENGINE MENGI KATIKA ELIMU YA SAYANSI YA MAPISHI, OFISI YANGU YA HEA INAKUPA MWANGA ZAIDI UJUE TATIZO LAKO KWA KINA NA SIO KUENDELEA KULALAMIKA.

Tumejifunza, Kinacho haribu mfumo wa chakula ni vyakula gani? Sukari na wanga. Je kinafanya Ini lizidiwe na mafuta na kufa ni nini? Sukari wanga na pombe. Je nini kingine kinacho haribu mfumo wa chakula Mafuta yenye kiwango kingi cha omega 6. Hayo ndio maadui wakushughulikia kama Unataka kurudisha nuru ya macho kwa kuongeza Vitamin A kama umeambiwa umepungukiwa. Kunywa galoni za karoti na matembele itakuwa kazi bure usiposhugulikia hivyo.

Elimu hio nadhani Itakusaidia sana.
𝐍𝐁📚:

Nakushauri kupata Kitabu cha 𝗦𝗮𝘆𝗮𝗻𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗛𝗼𝗺𝗼𝗻𝗶 𝗻𝗮 𝗨𝗴𝘂𝗺𝗯𝗮, ni kitabu kinachotoa elimu juu ya afya ya uzazi na magonjwa ya uzazi ikiwemo mvurugiko wa homoni, ugumba, uvimbe kwenye kizazi na magonjwa mbalimbali ya uzazi. Pia kinatoa mwongozo wa kula kiafya Ili kuepukana na magonjwa ya uzazi ikiwemo mvurugiko wa homoni.

KWA USHAURI NA MATIBABU 

 Karibu 𝗡𝘀𝗮𝗺𝗯𝗼 𝗛𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵𝗰𝗮𝗿𝗲 tupo mkabala na 𝗵𝗼𝘀𝗽𝗶𝘁𝗮𝗹𝗶 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝘆𝗮𝗺𝗮𝗹𝗮.

 Tupigie 𝟬𝟳𝟲𝟳𝟬𝟯𝟬𝟭𝟲𝟬

Karibu Nsambo Healthcare kupata huduma za kimatibabu n aushauri wa Lishe Bora.

kumbo, 0767074124

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *