𝐖𝐀𝐓𝐔 𝐇𝐀𝐖𝐀 π–π€ππŽ π‡π€π“π€π‘πˆππˆ πŠπ”ππ€π“π€ πŒπ€π†πŽππ‰π–π€ 𝐒𝐔𝐆𝐔 π˜π€ π‹πˆπ’π‡π„

wasiokula vyakula vya wanyama wako hatarini kupatwa na magonjwa sugu ya lishe 5

Ushawahi Kusikia Ukitaka kuwa na afya njema kuwa VEGAN yaani Mtu anayekula Vyakula vinavyotokana na Mimea tu yani, hali nyama kabisa.

Vegan ni taasisi yenye watu wachache tu duniani ila ina nguvu sana. Taasisi hii ilifanikiwa hadi sera zake za Lishe kuingizwa katika miongozo ya ushauri.

Ushawahi kusikia mtu anakwambia β€œMimi sili Nyama Samaki Kuku mayai? Nakula nafaka, Mizizi,mboga za majani na matunda tu? ” Hawa tunao lakini bado β€œHuwa nakutana nao clinic wana Kitambi, Kisukari,Shinikizo la damu, Magonjwa ya mifupa nk.

Huwa natafakari bila jibu kamili, hivi inakuwaje unaishi kwa Kuepuka vyakula vya wanyama lakini bado unakabiliwa na magonjwa sugu na hustuki yawezakuwa sio njia sahihi ya kula kiafya?

Kuna siku moja nilikutana na β€œMgonjwa mmoja kisukari kimemchakaza sana, Nikamshauri Ale kuzingatia kanuni zangu za @sayansiyamapishi . Akasema β€œSiwezi Kuacha wali maharage naupenda sana” Ila pia sili vitu vyote vya wanyama. Na kila mara anazidiwa na kupelekwa India kwa sababu ya sukari Kupanda.

protein sources concept, top view or flat lay

SIO SAHIHI KUTOKULA VYAKULA VYA WANYAMA
1. Binadamu mfumo wake wa Chakula haufanani na Mfumo wa Mifugo inayokula nyasi. Binadamu hawezi kusaga Mimea kwa wepesi kama Mifugo ambayo hadi Hucheua ili kukisaga zaidi.
Sisi sio wamajani…

2. Ukitazama kinywa cha binadamu kuna meno yaliyo chongoka pembeni huitwa Canine Teeth kazi yake ni β€œKukata kitu kigumu kama nyama” na sio Ugali wali ndizi Juisi tambi nk.

3. Enzi za kale nafaka tulikula kwa uchache sababu tulikuwa na nyenzo duni za kilimo na nyenzo duni za kusindika mahindi mtama na ngano kuwa unga. Tulitumia mawe kusaga. Huwezi lisha familia. Chakula kikuu kilitokana na β€œuwindaji,Ufugaji na Uvuvi”

5. Ukisikia β€œSuperfoods” au β€œNutrient dense foods” yaani vyakula vyenye Virutubisho vingi ni β€œNyama,samaki,kuku,mayai” na sio Wali,Ugali,ndizi,viazi tambi nk

6. Wagonjwa wangu wengi hupona kwa kuwaachisha vyakula visivyo na virutubisho na kuwaambia wale 75% vyenye virutubisho miezi 4-6 huku nikiwaongezea walivyo pungukiwa kwa miaka yote waliokula bila kujua. Muda wa siku 120 hunisimulia ushuhuda mkubwa sana ktk mwili.

7. Vegan anakwambia Asilimia 55-60 ya unachokula kiwe ni β€œWanga na sukari” na asilimia inayofuata ni Protini halafu mafuta hupigwa vita sana. Hivyo chakula chake kinakuwa ASILIMIA KUBWA KINA UHABA WA VIRUTUBISHO AKILA HIVYO MIAKA LAZIMA AFYA YAKE IKONGOROKE.

8. Usipokula vyakula vya wanyama lazima kila siku iendayo kwa Mungu ule Virutubisho katika mfumo wa Kidonge la sivyo utaugua upungufu wa hivyo virutubisho. Mfano Vitamin A, D, E ,K , Omega 3, na Vitamin B12. Makopo ya hizi dawa ni bei kubwa sana Huwezi kutumia Milele.
β€œNjia rahisi ni kubadilisha muundo wa sahani ili virutubisho hivyo Uvipate kwenye Sahani ya chakula unachokula kila siku”

9. Kuwa Vegan hakumfai kila mtu. Ndio maana kuna watu ni vegan ila wana Kitambi, Kisukari nk. Sasa Inakuwaje anapata kitambi wakati hanywi Pombe, Hali vyakula vya mafuta? Hapa ni Adui yupo kwenye sahani yake.

Kiufupi tu β€œKama unavyoishi unazidi kunenepa na kuumwa basi mwili wako haukustahili kula jinsi unavyokula”

whatsapp image 2025 11 06 at 09.52.11

UNAWEZA JIUNGA NA MASOMO YANGU KWA KUTUMA UJUMBE KWENYE INBOX β€œLISHE BORA 2026”

 SHARE WATU WAPONE NAOMBA NIPATE SHARES 100 LEO NITASHUSHA MAKALA NYINGINE NZITO

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *