𝗙𝗜𝗞𝗥𝗔 𝗛𝗔𝗦𝗜 𝗞𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗞𝗜𝗧𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗡𝗔 𝗨𝗭𝗜𝗧𝗢 𝗠𝗞𝗨𝗕𝗪𝗔

kitambi

Kunatafiti na fikra hasi mbalimbali ambazo zinazoelezea kuhusiana na kitambi. Fikra hizo zinawafanya watu wasiweze kudhibiti kitambi na uzito mkubwa na kuangukia kwenye magonjwa ya lishe.

Huu ndo ukweli kuhusu fikra za kitambi na uzito mkubwa;

𝗞𝗜𝗧𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗛𝗔𝗞𝗜𝗥𝗜𝗧𝗛𝗜𝗪𝗜

Binadamu hariithi kitambi, kisukari au pumu bali kinachorithiwa ni muundo wa mwili kibaiyolojia. Mtoto anazaliwa akiwa hana kitambi lakini ana muundo wa kuathirika na vyakula na mtindo wa maisha.

Tunarithi mfumo wa maisha ambao wazazi wetu wamepitia kama unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara au ulaji wa vyakula vya wanga na sukari ambavyo vinawaathiri miili yao kwa wepesi na kupata kitambi na uzito mkubwa.

Kwa mfano mama mjamzito mwenyeuzito mkubwa anamhatarisha mtoto aliyepo tumboni kuathirika na magonjwa yanayosababishwa na uzito mkuwa kama pumu, kisukari n.k.

A man in a red shirt holding his midsection, focusing on health issues.

𝗞𝗜𝗧𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗛𝗔𝗞𝗜𝗧𝗢𝗞𝗔𝗡𝗜 𝗡𝗔 𝗨𝗟𝗔𝗙𝐈 𝗔𝗨 𝗨𝗩𝗜𝗩𝗨

Pia kitambi hakisababishwi na ulafi au uvivu bali kitambi ndicho kinacholeta uvivu na ulafi. Kadri uzito unavyo ongezeka unahatarisha mafuta kukaa chini ya ngozi, mafuta kukaa kwenye viungo vya ndani kama vile ini na moyo ambayo yanasababisha uchovu wa kudumu.

Lakini pia kadiri uzito unavyoongezeka unasababisha mwili kushindwa kuratibu matumizi ya sukari na hali hiyo inasababisha mtu kupata njaa za mara kwa mara na kuwa na njaa kali au kupata dalili za vidonda vya tumbo.

Hayo yote ni matokeo ya kuwa na uzito mkubwa na kitambi na sio visababishi vya mtu kupata kitambi au uzito mkubwa.

Jifunze zaidi; bonyeza link hii 👇

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *