𝐌𝐖𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐔𝐉𝐀𝐀 𝐒𝐔𝐌𝐔

oxidative stress

𝐔𝐭𝐚𝐣𝐮𝐚𝐣𝐞 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐦𝐰𝐢𝐥𝐢 𝐰𝐚𝐤𝐨 𝐮𝐦𝐞𝐣𝐚𝐚 𝐒𝐔𝐌𝐔. (𝐎𝐱𝐢𝐝𝐚𝐭𝐢𝐯𝐞 𝐒𝐭𝐫𝐞𝐬𝐬)

Oxidative stress ni hali ya mwili kuwa katika msongo wa sumu zinazotokana na mabaki ya  oksijen mwilini ambazo zinajeruhi mwili.

Kunambinu mbalimbali za kimaabara ambazo zinaweza kukusaidia kutumika kujua kama mwili wako upo katika msongo wa mabaki ya oksijeni.

𝐍𝐣𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐊𝐮𝐣𝐢𝐜𝐡𝐮𝐧𝐠𝐮𝐳𝐚 𝐊𝐚𝐦𝐚 𝐔𝐧𝐚𝐬𝐮𝐦𝐛𝐮𝐥𝐢𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐠𝐨𝐧𝐣𝐰𝐚.

Kuna baadhi ya magonjwa yanaweza kuashiria kwamba mwili wako upo katika Oxidative Stress.

Magonjwa kama pumu ya kifua, yani kubanwa kifua katika nyakati tofauti  yaweza kuashiria kama mwili wako upo katika  msongo wa mabaki ya oksijeni, lakini pia magonjwa ya viungo kama vile baridi yabisi au baridi moto pia yaweza kuashiria kama mwili wako upo katika  msongo wa mabaki ya oksijeni.

Pia maradhi kama shinikizo la damu, kukosa nguvu za kiume, maumivu makali wakati wa hedhi, mvurugiko wa homoni kwa wanawake, magonjwa ya ngozi kama vile ngozi kuwasha, ngozi kututumka yaweza kuashiria kama mwili wako upo katika  msongo wa mabaki ya oksijeni.

Magonjwa hayo yote yanaashiria kama mwili wako unapata majeraha makali sana na kunakitu  kinaustua ndani ya mwili.

Hiyo ni njia ya kujifanyia utathmini kutokana na dalili ulizonazo ili kujua jinsi gani mwili wako unapata mashambulizi. Kwahiyo unapoona dalili za hayo magonjwa ni vyema kuwahi kituo cha afya ili kuanza matibabu.

oxidative stress 1024x822 1 600x482

𝐍𝐣𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐮𝐦𝐢𝐚 𝐒𝐚𝐦𝐩𝐮𝐥𝐢 𝐳𝐚 𝐃𝐚𝐦𝐮 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐚𝐛𝐚𝐫𝐚.

Daktari anaweza kutathmini ni kwa kiasi gani mwili wako umepata mashambulizi kwa kutumia sampuli za damu. Tafiti zinaonyesha kwamba kipimo cha 𝑪-𝒓𝒆𝒂𝒄𝒕𝒊𝒗𝒆 𝑷𝒓𝒐𝒕𝒊𝒏  kinaweza kutathmini jinsi gani mwili wako umepata mashambulizi yanayotokana na mwili kuwa katika msongo wa mabaki ya oksijen

Kipimo hiki kinaenda sambamba na kipimo cha 𝑯𝒊𝒈𝒉 𝒔𝒆𝒏𝒔𝒊𝒕𝒊𝒗𝒊𝒕𝒚 𝑪-𝒓𝒆𝒂𝒄𝒕𝒊𝒗𝒆 𝑷𝒓𝒐𝒕𝒊𝒏. Kipimo ambacho ni kiashiria ya kwamba mishipa ya damu ipo hatarini kupata majeraha makubwa au moyo upo hatarimi kupata shambulio la moyo.

𝑯𝒊𝒈𝒉 𝒔𝒆𝒏𝒔𝒊𝒕𝒊𝒗𝒊𝒕𝒚 𝑪-𝒓𝒆𝒂𝒄𝒕𝒊𝒗𝒆 𝑷𝒓𝒐𝒕𝒊𝒏 inaweza kupanda kama mtu unawiki chache baada ya kuumwa magonjwa kama U.T.I au umepata homa kali inayoweza kusababisha mwili umepata majeraha.

Lakini endapo mtu hakuumwa ugonjwa wowote hivi karibuni na akipimwa kipimo cha  𝑯𝒊𝒈𝒉 𝒔𝒆𝒏𝒔𝒊𝒕𝒊𝒗𝒊𝒕𝒚 𝑪-𝒓𝒆𝒂𝒄𝒕𝒊𝒗𝒆 𝑷𝒓𝒐𝒕𝒊𝒏  kukutwa ipo juu, hali hiyo inaashiria ya kwamba  mwili upo hatarini na umepata majeraha makali kutokana na mashambulio makali sana.

Kwa wale wagonjwa wengi wenye uzito mkubwa yale mafuta ya ziada yanayoukalia mwili  yanatizamwa kama kivamizi ndani ya mwili na kuanza mpambano unaosababisha 𝑪-𝒓𝒆𝒂𝒄𝒕𝒊𝒗𝒆 𝑷𝒓𝒐𝒕𝒊𝒏 kuwa juu.

Hata kwa wagonjwa wa kisukari, mwili unapolemewa na sukari nyingi huwa unazalisha mamabaki ya oksijeni kwa wingi sana. Kwahiyo mgonjwa wa kisukari anatakiwa kufanyiwa kipimo cha 𝑯𝒊𝒈𝒉 𝒔𝒆𝒏𝒔𝒊𝒕𝒊𝒗𝒊𝒕𝒚 𝑪-𝒓𝒆𝒂𝒄𝒕𝒊𝒗𝒆 𝑷𝒓𝒐𝒕𝒊𝒏 ili kumsaidia kushusha sukari kwa kutumia chakula ili kuzuia kupata mashambulizi kwenye viungo vya mwili.

Madaktari wengi huwa wanasahau kufanya kipimo hiki. Kwahiyo wewe mgonjwa unayesumbuliwa na kisukari, shinikizo la damu, pumu ya kifua na pumu ya ngozi, unatakiwa kufuatilia na kufanya kipimo hiki kitakachokusaidia kupata majibu ya tatizo lako kwasababu huenda mwili wako umejawa na mabaki ya sumu za  oksijeni.

Jifunze zaidi; bonyeza link hii 👇

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *