Kupungua kiafya maana yake mfumo unaotumka ni ule ambao bado unaoupatia mwili viinilishe vyote kama mafuta, wanga, protini na madini ili kusaidia mwili kuendelea na shughuli zake za ndani bila ngozi kulegea.
Kupungua kwa maradhi ni kule kupungua huku muonekano wako unaharibika kama kukonda, ngozi inayovutika, ngozi imelegea n.k .
kupungua kwa maradhadhi kunasababishwa na;
𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗿𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗮.
Mtu unapodhoofika mara kwa mara bila sababu za msingi inawezekana kuwa na magonjwa ya kuambukiza yanakufanya upungue. Kwahiyo ni vyema kuwahi kituo cha afya ili kupata majibu kamili na kuanza matibabu.

𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝘂𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗧𝘂𝗯𝗲𝗿𝗰𝘂𝗹𝗼𝘀𝗶𝘀 (𝗧𝗕).
Kama unapungua kunaambatana na jotokali, kikohozi au kupoteza uzito kwa kasi. ni vyema kuwahi kituo cha afya ili kuanza matibabu.nawezekana kupungua kwako kunaambatana na tb kutokana na jotokali wakati wa usiku
𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗿𝗮𝗱𝗵𝗶 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗳𝘂𝗺𝗼 𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮.
Magonjwa kama vidonda vya tumbo yanasababisha maumivu makali unapokula chakula, kupata gesi na kuharisha. Hali hiyo inasababisha mtu kuogopa kula chakula na matokeo yake mwili unaanza kudhoofika na kupungua kwasababu ya kukosa viinilishe.
𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝘂𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝘀𝗮𝗿𝗮𝘁𝗮𝗻𝗶 (𝗰𝗮𝗻𝗰𝗲𝗿).
Ugonjwa wa kansa unasababisha mtu kupungua kwa kasi kutokana na mtu kuwa na msongo wa mawazo unaosababisha kukosa hamu ya kula.

𝗞𝘂𝘁𝗮𝗸𝗮 𝗸𝘂𝗽𝘂𝗻𝗴𝘂𝗮 𝘂𝘇𝗶𝘁𝗼 𝗸𝘄𝗮 𝗻𝗴𝘂𝘃𝘂.
Kuna watu wanapungunguza uzito kwa nguvu kutokana na muonekano wao na jinsi watu wanavyowaongelea. Hali hiyo inawafanya kupunguza uzito kwa mabavu kwa kujinyima kula chakula.
Mwili wa binadamu unahitaji vyakula vya mafuta na wanga ili upate nguvu. Panapokuwepo na mafuta na wanga mwili huchagua kutumia wanga zaidi kuliko mafuta. Inapotokea mwili umekosa wanga, utachagua njia mbadala ambayo ni protini ili kujitengenezea nishati.
Kwahiyo protini inavyotumiwa na mwili ili kutengeneza nishati, inaunguza protini ya kwenye misuli na kusababisha misuli kulegea nyama zinatepeta. Hiyo ni kwasababu mwili wako umeunyima ainazote za vyakula vya wanga na protini.
Kwahiyo sikushauri ujinyime chakula ili upunguze uzito au kitambi. Kupungua uzito sio swala la mabavu ni swala la kutumia akili kwa kujifunza sayansi ya kutumia chakula ambayo ni Sayansi ya Mapishi.
Jifunze zaidi; bonyeza link hii


