Tezi ya shingoΒ (thyroid)Β ni tezi inayopatikana katika eneo la shingo ambayo inamwaga homoni zake ambazo ni thyroxine (T4) na triiodothyronine (T3) kwenye damu zenye kazi ya kuratibu mchakato wa kazi za kimetaboliki mwilini.
Tezi ya shingo ikishindwa kufanya kazi yake vizuri na kufanya kazi kinyume na kawaida mwilini, mwili utapata ugonjwa wa goita ambao umegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Hyperthyroidism
Huu ni ugonjwa ambao tezi ya shingo inamwaga homoni zake kwa kiwango cha juu sana katika damu zaidi ya kiwango kinachotakiwa.
Endapo homoni za tezi ya shingo zitamwagwa nyingi katika damu, basi mgonjwa ataonyeha dalili zifuatazo;
- Mapigo ya moyo kwenda mbio zaidi
- Mzunguko mbaya wa hedhi
- Kukonda au mwili kupungua kwa kasi
- Kukosa usingizi na kushindwa kulala
- Joto la mwili kuongezeka na kuhisi kuungua
- Mwili kuishiwa nguvu
- Kuwa na hasira za mara kwa mara
- Nywele na kucha kukatika
- Ngozi kuwa nyembamba
- Hyporthyroidism
Huu ni ugonjwa ambao tezi ya shingo inamwaga homoni zake kwa kiwango cha chini sana katika damu zaidi ya kiwango kinachotakiwa.
Endapo homoni za tezi ya shingo zitamwagwa kwa kiasi kidogo katika damu, basi mgonjwa ataonyeha dalili zifuatazo;
- Mwili kuwa na uchovu na ushaifu kupitiliza
- Mwili kunenepa sana
- Sauti kuwa nzito
- Misuli kukaza
- Msongo wa mawazo
- Kupata choo kigumu
Matatizo katika tezi ya shingo na magonjwa ya goita yanasababishwa na mambo mafuatayo
- Upungufu wa madini ya chuma
- Sumu za zitokanazo na vyakula
- Mashambulio ya kinga ya mwili
Tafiti za kisayansi zinaonyesha kwamba asilimia kubwa ya wagonjwa wa goita ni wanawake kuliko wanaume hali hiyo inasababishwa na maumbo ya kibaiyolojia kati ya mwanamke na mwanaume. Kitendo cha mwanamke kuingia hedhi kila mwezi kinamsababishia kupoteza madini chuma mwilini na endapo hatazingatia lishe bora basi mwanamke huyo anahatari zaidi ya kupata ugonjwa wa goita.
Matibabu ya ugonjwa wa goita unatibika kulingana na aina tatizo na jinsi tatizo la mgonjwa lilivyofikia.
Jifunze zaidi; bonyeza link hii 


