Mtahiniwa wa ugonjwa wa kisukari ni mtu amabae mda wowote kuanzia sasa anaweza kutambulika na kubaikina rasmi kwamba anaugonjwa wa kisuakri na kunza dawa. Watu wengi sana wanatembea barabarani huku wakiwa ni watahiniwa wa ugonjwa wa kiskari bila kujitambua.
Mtahiniwa wa ugonjwa wa kisukari hawezi kubainika kwa kutumia kipimo kidogo kinachoitwa 𝐆𝐥𝐮𝐜𝐨𝐦𝐞𝐭𝐞𝐫, kwa maana hiyo wagonjwa wengi huwa wanagunduilika wakiwa tayari wameshafika hatua ya tatu ya ugonjwa wa kisukari.

Hizi ni mbinu kuu tatu za kujigunudua kama wewe ni mtahiniwa wa ugonjwa wa kisuari;
𝟏. 𝐏𝐢𝐦𝐚 𝐬𝐮𝐤𝐚𝐫𝐢 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐚𝐬𝐮𝐛𝐮𝐡𝐢 𝐤𝐚𝐛𝐥𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐭𝐮 𝐜𝐡𝐨𝐜𝐡𝐨𝐭𝐞.
Endapo sukari yako ikisoma zaidi ya 6.1 mpaka 7 mmol/L basi wewe ni mtahiniwa wa ugonjwa wa kisukari na unaitwa rasmi una 𝐈𝐦𝐩𝐚𝐫𝐞𝐝 𝐅𝐚𝐬𝐭𝐢𝐧𝐠 𝐁𝐥𝐨𝐨𝐝 𝐆𝐥𝐮𝐜𝐨𝐬𝐞.
𝟐. 𝐍𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐤𝐢𝐭𝐮𝐨 𝐜𝐡𝐚 𝐚𝐟𝐲𝐚.
Daktari anatakiwa akufanyie kipimo kinaitwa 𝐎𝐫𝐚𝐥 𝐆𝐥𝐮𝐜𝐨𝐬𝐞 𝐓𝐨𝐥𝐞𝐫𝐚𝐧𝐜𝐞, hiki ni kipimo cha kuchokoza mwili wako na donge la sukari la gm 75. Baada ya kipimo hiko sukari yako inatakiwa isome chini ya 7 baada ya masaa mawili. Endapo sukari yako ikisoma kuanzia 7 mpaka 11.1 tafsiri yake ni kwamba umeanza kupata 𝐈𝐦𝐩𝐚𝐫𝐞𝐝 𝐆𝐥𝐮𝐜𝐨𝐬𝐞 𝐓𝐨𝐥𝐥𝐞𝐫𝐚𝐧𝐜𝐞 𝐓𝐞𝐬𝐭 kwa maana hiyo unahesabika kama mtahiniwa wa ugonjwa wa kisukari.
𝟑. 𝐊𝐮𝐩𝐢𝐦𝐚 𝐚𝐭𝐡𝐚𝐫𝐢 𝐳𝐚 𝐬𝐮𝐤𝐚𝐫𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐝𝐚𝐦𝐮.
Kabla hujawa mgonjwa rasmi wa kisukari, sukari huwa inatumia muda mrefu sana kushuka. Ile sukari inayotumia muda mrefu zaidi ya masaa mawili kushuka sana kushuka huleta athari katika mishipa ya damu na kwenye mwili kwa ujumla. Kiwango cha uharibifu huwa kinapimwa na kipimo kinachoitwa 𝐆𝐥𝐲𝐜𝐨𝐬𝐲𝐥𝐚𝐭𝐞𝐝 𝐇𝐞𝐦𝐨𝐠𝐥𝐨𝐛𝐢𝐧 ambacho kinapima kiwango cha seli nyekundu za damu zilizoharibiwa na sukari. Endapo kipimo hiko cha kikisoma 5.7% mpaka 6.4% unahesabika rasmi kama mgonjwa wa kisukari.
Jifunze zaidi; bonyeza link hii
𝐍𝐁:
Nakushauri kupata Kitabu cha 𝗦𝗮𝘆𝗮𝗻𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗠𝗮𝗽𝗶𝘀𝗵𝗶. Kitabu kinatoa elimu ya magonjwa ya lishe, elimu ya sayansi ya vyakula sahihi kwa afya na mpangilio wa chakula utakaokusaidia kuondokana na magonjwa ya lishe kama kisukari, kitambi na uzito mkubwa, shinikiizo la damu upungufu wa nguvu za kiume n.k.
KWA USHAURI NA MATIBABU
Karibu 𝗡𝘀𝗮𝗺𝗯𝗼 𝗛𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵𝗰𝗮𝗿𝗲 tupo mkabala na 𝗵𝗼𝘀𝗽𝗶𝘁𝗮𝗹𝗶 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝘆𝗮𝗺𝗮𝗹𝗮.
Tupigie 𝟬𝟳𝟲𝟳𝟬𝟯𝟬𝟭𝟲𝟬


