𝐍𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐒𝐈𝐎 𝐌𝐁𝐎𝐆𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐒𝐈𝐎 𝐌𝐋𝐎 𝐌𝐊𝐔𝐔

wanga si mlo mkuu 768x432

Ni tamaduni zetu kwa sasa vyakula vya wanga na sukari kutawala katika sahani zetu, hali imekua ikituhumiwa na tafiti nyingi kwamba inaleta magonjwa ya uzazi, kitambi,shinikizo la damu na magonjwa mengi.

Mbali na kwamba watu wanakula vyakula vya wanga na sukari katika sahani kilasiku, madoido ya upishi pia yanachangia sana watu kuumwa magonjwa ya lishe.

Si watu wote wanastahili kiwango kikubwa cha wanga katika sahani.Tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya aslimia 60 katika jamii haistahimili kiasi kikubwa cha wanga na sukari, lakini cha ajabu mpangilio wa kula ndo umejaa vyakula vya wanga na sukari.

wanga ulyclinic

Ikiwa mwili wako haustahimili vyakula vya wanga na sukari kwa wingi, utaanza kuonyesha magonjwa ya kutostahimili vyakula vya wanga na sukari mapema ikiwemo kitambi, kisukari, shinikizo la damu, kansa, ugumba, uvimbe kwenye kizazi n.k

𝑺𝒂𝒃𝒂𝒃𝒖 𝒌𝒖𝒖 𝒌𝒘𝒂𝒏𝒊𝒏𝒊 𝒗𝒚𝒂𝒌𝒖𝒍𝒂 𝒗𝒚𝒂 𝒘𝒂𝒏𝒈𝒂 𝒏𝒂 𝒔𝒖𝒌𝒂𝒓𝒊 𝒉𝒂𝒗𝒊𝒕𝒂𝒌𝒊𝒘𝒊 𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒎𝒍𝒐 𝒎𝒌𝒖𝒖;
 𝗩𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝘃𝘆𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗴𝗮 𝗻𝗮 𝘀𝘂𝗸𝗮𝗿𝗶 𝘃𝗶𝗻𝗮𝘂𝗵𝗮𝗯𝗮 𝘄𝗮 𝘃𝗶𝗿𝘂𝘁𝘂𝗯𝗶𝘀𝗵𝗼.
Katika makundi makubwa matatu ya vyakula vya wanga, mafuta na protini, vyakula vya wanga ndivyo ambavyo vinauhaba mkubwa wa virutubisho.

Katika makundi haya ya vyakula, mwili huwa unahitaji virutubisho vya ziada na sio sukari ya ziada ndio maana mwili wa binadamu haustahimili kiwango kikubwa cha sukari.

𝗩𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝘃𝘆𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗴𝗮 𝘃𝗶𝗻𝗮𝗹𝗲𝘁𝗮 𝘂𝗿𝗮𝗶𝗯𝘂 𝗮𝘂 𝘂𝘁𝗲𝗴𝗲𝗺𝗲𝘇𝗶.
Vyakula hivi vinaathiri uwezo wa ubongo kutofanya kazi vizuri, ni sawasawa na watu wanaovuta sigara, wanaokunywa pombe huwa vinaharibu mfumo ya ubongo sawasawa na vyakula vya wanga. Unapokuwa mraibu unakuwa hauwezi kujikadiria kiasi lazima utakula kupindukia na jinsi unavyokula kiasi kikubwa ndivyo unavyohisi kuburudika ka kukaribisha magonjwa .

high carb foods 2

𝗩𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝘃𝗶𝗻𝗮𝗹𝗲𝘁𝗮 𝗻𝗷𝗮𝗮 𝗵𝗮𝗿𝗮𝗸𝗮.
Vyakula hivi vinaleta nja haraka kwasababu vinapandisha sukari haraka ndani ya muda mfupi. Jaribu kula vyakula ambavyo utakaa kwa mda mrefu bila kuhisi njaa. Ili uweze kufanikiwa hilo zoezi lazima upunguze vyakula vya wa na sukari katika sahani yako.

𝗩𝗶𝗻𝗮𝘇𝘂𝗶𝗮 𝗸𝘂𝗽𝘂𝗻𝗴𝘂𝗮 𝘂𝘇𝗶𝘁𝗼 𝗻𝗮 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶 𝗸𝘂𝗳𝗮𝗻𝘆𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗲𝗻𝗴𝗲𝗻𝗲𝘇𝗼.
Njia za kufanya matengeeno zipo mbili ambazo ni kufunga au kupunguza vyakula vya wanga na sukari katika sahani yako. Vyakula hivi ili viweze kutumika mwilini huwa vinahamasisha kongosho kutema homoni ya insulin ambayo huwa inazuia usipungue uzito au kufanya matengenezo. Kwahiyo ili kujipeusha na magonjwa ya uchakavu wa mwilii basi punguza vyakula vya wanga na sukari.

Unauwezo wa kupunguza au kuacha kutumia hivyo vya vyakula kama utafuata muongozo wa  kitabu cha Sayansi ya mapishi ili uweze kupangilia mfumo wako wa vyakula ambavyo utatakiwa kula na vyakula vitakavyokuondolea uraibu wa kula wanga na sukari ili kujilinda na magonjwa ya lishe.

Jifunze zaidi; bonyeza link hii 

NB
Nakushauri kupata Kitabu cha 𝗦𝗮𝘆𝗮𝗻𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗠𝗮𝗽𝗶𝘀𝗵𝗶, ni mwongozo wa kula kiafya utakaokusaidia kuondokana na magonjwa ya mfumo wa chakula kwa kufuata mpnaglilio wa lishe bora na kuimarisha afya yako Ili kuepukana na magonjwa mengine ya lishe ikiwemo kisukari, kitambi na uzito mkubwa, shinikiizo la damu upungufu wa nguvu za kiume n.k.

Kitabu kinatoa elimu ya manunuzi, elimu ya magonjwa ya lishe, elimu ya vyakula sahihi kwa afya na mpangilio wa chakula.

KWA USHAURI NA MATIBABU

📍 Karibu 𝗡𝘀𝗮𝗺𝗯𝗼 𝗛𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵𝗰𝗮𝗿𝗲 tupo mkabala na 𝗵𝗼𝘀𝗽𝗶𝘁𝗮𝗹𝗶 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝘆𝗮𝗺𝗮𝗹𝗮.

☎️ Tupigie 𝟬𝟳𝟲𝟳𝟬𝟯𝟬𝟭𝟲𝟬

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *