𝐒𝐀𝐁𝐀𝐁𝐔 𝐙𝐀 𝐔𝐕𝐈𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐊𝐈𝐙𝐀𝐙𝐈

uvimbe kizazi 768x432

Mji wa mimba ni sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke ambayo imeunganishwa na mirija ya uzazi inayosaidia kubeba mayai kutoka kwenye ovari hadi kwenye mji wa mimba sehemu ambayo kijusi hukua.

Sehemu ya chini ya mji wa mimba inaunganishwa na uke na inaitwa 𝒔𝒆𝒗𝒊𝒌𝒔𝒊, sehemu pana ya juu zaidi ya uterasi ambapo mirija ya uzazi huungana inaitwa  𝑭𝒖𝒏𝒅𝒖𝒔 na mji mkuu wa mimba  ambapo yai lililorutubishwa hukua kipindi cha ujauzito huitwa  𝑪𝒐𝒓𝒑𝒖𝒔.

𝐓𝐚𝐛𝐚𝐤𝐚 𝐳𝐚 𝐦𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐦𝐢𝐦𝐛𝐚;
𝑬𝒏𝒅𝒐𝒎𝒆𝒕𝒓𝒊𝒂𝒎𝒖; Huu ni ukuta wa ndani wa kizazi ambapo yai liliolorutubishwa hujishikiza na kutengeneza kijusi mpaka kukua lakini pia hujisafisha kila baada ya mwezi na kufanya mwanamjke apate hedhi endapo kama hakuna yai lililorutubishwa.

𝑴𝒊𝒐𝒎𝒆𝒕𝒓𝒊𝒂𝒎𝒖; Hii ni safu nene ya misuli ya kati ya corpus au fundus inayopanuka wakati wa ujauzito ili kushikilia mtoto anayekua na inapunguza wakati wa mwanamke kujifungua ili kusukuma mtoto nje.

𝑺𝒆𝒓𝒐𝒔𝒂; Hii ni safu laini ya nje. Hufunika mji wa mimba na kurahisisha mjiwa mimba kuteleza na kusogea ndani ya pelvisi inapohitajika.

picture1


𝑼𝒗𝒊𝒎𝒃𝒆 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒌𝒊𝒛𝒂𝒛𝒊 ni uvimbe wa misuli usiokuwa wa saratani ambayo hukua kwenye ukuta wa mji wa mimba au uterasi.

𝑲𝒖𝒏𝒂 𝒂𝒊𝒏𝒂 𝒕𝒐𝒇𝒂𝒖𝒕𝒊 𝒛𝒂 𝒖𝒗𝒊𝒎𝒃𝒆 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒌𝒊𝒛𝒂𝒛𝒊  𝒌𝒖𝒍𝒊𝒏𝒈𝒂𝒏𝒂 𝒏𝒂 𝒔𝒆𝒉𝒆𝒎𝒖 𝒛𝒊𝒏𝒂𝒑𝒐𝒌𝒖𝒂 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒎𝒋𝒊 𝒘𝒂 𝒎𝒊𝒎𝒃𝒂.

1. 𝑺𝒖𝒃𝒔𝒆𝒓𝒐𝒖𝒔 𝒂𝒖 𝒔𝒖𝒃𝒔𝒆𝒓𝒐𝒔𝒂𝒍 𝒇𝒊𝒃𝒓𝒐𝒊𝒅𝒔 hukua kwenye ukuta wa nje wa safu ya misuli.

2. 𝑺𝒖𝒃𝒎𝒖𝒄𝒐𝒔𝒂𝒍 𝒇𝒊𝒃𝒓𝒐𝒊𝒅𝒔 ni uvimbe kwenye kizazi  ambao hukua kwenye ukuta wa misuli ya mji wa mimba kwa ndani.


Uvimbe kwenye kizazi ambao sio wa saratani ni mbaya sana kwasababu unaweza kukua kama uvimbe mmoja, unaweza kuwa mdogo mdogo uliotawanyika katika mji wa mimba.

𝐒𝐚𝐛𝐚𝐛𝐮 𝐲𝐚  𝐮𝐯𝐢𝐦𝐛𝐞 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐤𝐢𝐳𝐚𝐳𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐦𝐢𝐦𝐛𝐚.

Sababu ya  𝒖𝒗𝒊𝒎𝒃𝒆 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒌𝒊𝒛𝒂𝒛𝒊 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒎𝒋𝒊 𝒘𝒂 𝒎𝒊𝒎𝒃𝒂 haijulikani lakini homoni za kike estrojeni na homoni za projesteroni zimehusishwa katika ukuaji wauvimbe kwenye kizazi.

Kwa kawaida uvimbe kwenye kizazi hukua wakati wa miaka ya uzazi ambayo mwanamke anakuwa na uwezo wa kubeba mimba na uvimbe huo unaweza kusinyaa bada aya mwanamke kukoma hedhi.

𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐲𝐚 𝐡𝐚𝐭𝐚𝐫𝐢 𝐲𝐚𝐧𝐚𝐲𝐨𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐦𝐰𝐚𝐧𝐚𝐦𝐤𝐞 𝐤𝐮𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐮𝐯𝐢𝐦𝐛𝐞 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐤𝐢𝐳𝐚𝐳𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐦𝐢𝐦𝐛𝐚;

Θ 𝑴𝒕𝒐𝒕𝒐 𝒘𝒂 𝒌𝒊𝒌𝒆 𝒌𝒖𝒑𝒂𝒕𝒂 𝒉𝒆𝒅𝒉𝒊 𝒂𝒌𝒊𝒘𝒂 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒖𝒎𝒓𝒊 𝒎𝒅𝒐𝒈𝒐

.Θ 𝑴𝒂𝒕𝒖𝒎𝒊𝒛𝒊 𝒚𝒂 𝒅𝒂𝒘𝒂 𝒛𝒂 𝒖𝒛𝒂𝒛𝒊 𝒘𝒂 𝒎𝒑𝒐𝒂𝒈𝒐 𝒌𝒂𝒃𝒍𝒂 𝒚𝒂 𝒎𝒊𝒂𝒌𝒂 𝟏𝟔
.Θ  𝑴𝒂𝒕𝒂𝒕𝒊𝒛𝒐 𝒚𝒂 𝒗𝒊𝒏𝒂𝒔𝒂𝒃𝒂
.Θ  𝑼𝒏𝒆𝒏𝒆 𝒌𝒖𝒑𝒊𝒕𝒂 𝒌𝒊𝒂𝒔𝒊
.Θ  𝑼𝒍𝒂𝒋𝒊 𝒘𝒂 𝒗𝒚𝒂𝒌𝒖𝒍𝒂 𝒗𝒚𝒂 𝒌𝒖𝒌𝒂𝒂𝒏𝒈𝒂 𝒌𝒖𝒑𝒊𝒏𝒅𝒖𝒌𝒊𝒂.
.Θ  𝑼𝒏𝒚𝒘𝒂𝒋𝒊 𝒘𝒂 𝒑𝒐𝒎𝒃𝒆
.Θ  𝑯𝒊𝒔𝒕𝒐𝒓𝒊𝒂 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒇𝒂𝒎𝒊𝒍𝒊𝒂 𝒋𝒖𝒖 𝒚𝒂 𝒎𝒂𝒈𝒐𝒏𝒋𝒘𝒂 𝒚𝒂 𝒖𝒛𝒂𝒛𝒊
.Θ  𝑼𝒗𝒖𝒕𝒂𝒋𝒊 𝒘𝒂 𝒔𝒊𝒈𝒂𝒓𝒂

tp uva fibroids cartoon

𝐃𝐚𝐥𝐢𝐥𝐢 𝐳𝐚  𝐮𝐯𝐢𝐦𝐛𝐞 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐤𝐢𝐳𝐚𝐳𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐦𝐢𝐦𝐛𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐰𝐚𝐧𝐚𝐦𝐤𝐞 𝐧𝐢 𝐩𝐚𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐧𝐚:

.⇒ 𝑲𝒖𝒕𝒐𝒌𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒅𝒂𝒎𝒖 𝒏𝒚𝒊𝒏𝒈𝒊 𝒂𝒖 𝒎𝒂𝒖𝒎𝒊𝒗𝒖 𝒎𝒂𝒌𝒂𝒍𝒊 𝒘𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊 𝒘𝒂 𝒉𝒆𝒅𝒉𝒊.
.⇒  𝑲𝒖𝒑𝒂𝒕𝒂 𝒉𝒆𝒅𝒉𝒊 𝒛𝒂𝒊𝒅𝒊 𝒚𝒂 𝒎𝒂𝒓𝒂𝒎𝒃𝒊𝒍𝒊 𝒌𝒘𝒂 𝒎𝒘𝒆𝒛𝒊.
.⇒  𝑲𝒖𝒉𝒊𝒔𝒊 𝒕𝒖𝒎𝒃𝒐 𝒍𝒂 𝒄𝒉𝒊𝒏𝒊 𝒌𝒖𝒋𝒂𝒂 𝒈𝒆𝒔𝒊 𝒂𝒖 𝒌𝒖𝒗𝒊𝒎𝒃𝒂.
.⇒  𝑲𝒖𝒌𝒐𝒋𝒐𝒂 𝒎𝒂𝒓𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒎𝒂𝒓𝒂 (𝒉𝒊𝒊 𝒊𝒏𝒂𝒘𝒆𝒛𝒂 𝒌𝒖𝒕𝒐𝒌𝒆𝒂 𝒘𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊 𝑼𝒗𝒊𝒎𝒃𝒆
.⇒  𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒌𝒊𝒛𝒂𝒛𝒊  𝒖𝒏𝒂𝒘𝒆𝒌𝒂 𝒎𝒈𝒂𝒏𝒅𝒂𝒎𝒊𝒛𝒐 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒌𝒊𝒃𝒐𝒇𝒖 ).
.⇒  𝑴𝒂𝒖𝒎𝒊𝒗𝒖 𝒎𝒂𝒌𝒂𝒍𝒊 𝒘𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊 𝒘𝒂 𝒌𝒖𝒔𝒉𝒊𝒓𝒊𝒌𝒊 𝒕𝒆𝒏𝒅𝒐 𝒍𝒂 𝒏𝒅𝒐𝒂.
.⇒  𝑴𝒂𝒖𝒎𝒊𝒗𝒖 𝒚𝒂 𝒎𝒈𝒐𝒏𝒈𝒐 𝒔𝒆𝒉𝒆𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝒄𝒉𝒊𝒏𝒊 𝒚𝒂 𝒎𝒈𝒐𝒏𝒈𝒐.
.⇒  𝑲𝒖𝒑𝒂𝒕𝒂 𝒄𝒉𝒐𝒐 𝒌𝒊𝒈𝒖𝒎𝒖.
.⇒  𝑲𝒖𝒕𝒐𝒌𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒖𝒄𝒉𝒂𝒇𝒖 𝒖𝒌𝒆𝒏𝒊 𝒌𝒘𝒂 𝒎𝒖𝒅𝒂 𝒎𝒓𝒆𝒇𝒖.
.⇒  𝑲𝒖𝒕𝒐𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒖𝒘𝒆𝒛𝒐 𝒘𝒂 𝒌𝒖𝒌𝒐𝒋𝒐𝒂 𝒂𝒖 𝒌𝒖𝒎𝒂𝒍𝒊𝒛𝒂 𝒌𝒂𝒃𝒊𝒔𝒂 𝒎𝒌𝒐𝒋𝒐 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒌𝒊𝒃𝒐𝒇𝒖.
.⇒  𝑲𝒖𝒐𝒏𝒈𝒆𝒛𝒆𝒌𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒖𝒌𝒖𝒃𝒘𝒂 𝒘𝒂 𝒕𝒖𝒎𝒃𝒐 𝒏𝒂 𝒌𝒖𝒔𝒂𝒃𝒂𝒃𝒊𝒔𝒉𝒂 𝒕𝒖𝒎𝒃𝒐 𝒍𝒂𝒌𝒐 𝒌𝒖𝒐𝒏𝒆𝒌𝒂𝒏𝒂 𝒌𝒂𝒎𝒂 𝒎𝒋𝒂𝒎𝒛𝒊𝒕𝒐.

𝐌𝐚𝐝𝐡𝐚𝐫𝐚 𝐲𝐚 𝐮𝐯𝐢𝐦𝐛𝐞 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐤𝐢𝐳𝐚𝐳𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐦𝐢𝐦𝐛𝐚 𝐧𝐢:
♦ 𝑴𝒂𝒖𝒎𝒊𝒗𝒖 𝒎𝒂𝒌𝒂𝒍𝒊 𝒂𝒎𝒃𝒂𝒚𝒐  𝒉𝒂𝒚𝒂𝒘𝒆𝒛𝒊 𝒌𝒖𝒅𝒉𝒊𝒃𝒊𝒕𝒊𝒘𝒂.
♦ 𝑲𝒖𝒗𝒊𝒎𝒃𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒕𝒖𝒎𝒃𝒐.
♦  𝑲𝒖𝒕𝒐𝒌𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒅𝒂𝒎𝒖 𝒏𝒚𝒊𝒏𝒈𝒊  𝒘𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊 𝒘𝒂 𝒉𝒆𝒅𝒉𝒊.
♦  𝑼𝒑𝒖𝒏𝒈𝒖𝒇𝒖 𝒘𝒂 𝒅𝒂𝒎𝒖.
♦  𝑲𝒖𝒑𝒂𝒕𝒂 𝒖𝒈𝒖𝒎𝒃𝒂.

Matibabu ya  𝒖𝒗𝒊𝒎𝒃𝒆 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒌𝒊𝒛𝒂𝒛𝒊 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒎𝒋𝒊 𝒘𝒂 𝒎𝒊𝒎𝒃𝒂 yanafanyika kitaalamu katika kituo cha afya. Ninakushauri sana mara uonapo dalili za ugonjwa huu basi wahi katika kituo cha afya na kuanza matibabu ya haraka kabla hujapata madhara makubwa ikiwemo  ugumba.

𝐍𝐁📚:

Nakushauri kupata Kitabu cha 𝗦𝗮𝘆𝗮𝗻𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗛𝗼𝗺𝗼𝗻𝗶 𝗻𝗮 𝗨𝗴𝘂𝗺𝗯𝗮, ni kitabu kinachotoa elimu juu ya afya ya uzazi na magonjwa ya uzazi ikiwemo mvurugiko wa homoni, ugumba, uvimbe kwenye kizazi na magonjwa mbalimbali ya uzazi. Pia kinatoa mwongozo wa kula kiafya Ili kuepukana na magonjwa ya uzazi ikiwemo mvurugiko wa homoni.

KWA USHAURI NA MATIBABU

📍 Karibu 𝗡𝘀𝗮𝗺𝗯𝗼 𝗛𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵𝗰𝗮𝗿𝗲 tupo mkabala na 𝗵𝗼𝘀𝗽𝗶𝘁𝗮𝗹𝗶 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝘆𝗮𝗺𝗮𝗹𝗮.

☎️ Tupigie 𝟬𝟳𝟲𝟳𝟬𝟯𝟬𝟭𝟲𝟬

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *