𝐌𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐌𝐁𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐙𝐈𝐓𝐎 𝐌𝐊𝐔𝐁𝐖𝐀

punguza kitambi 768x432

Watu wengi hujitapa kwamba uzito wao hauwaathiri afya zao. uzito mkubwa huwa havileti madhara kw amuda mfupi, kadri unavyokaa na uzito mkubwa ndivyo maradhi sugu yanavyozidi kujijenga katika mwili wako.

fat person

Madhara ya uzito mkubwa na kitambi.

🚨 𝗩𝗶𝘂𝗻𝗴𝗼 𝗸𝘂𝘀𝗮𝗴𝗶𝗸𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗶𝗴𝘂𝘂 𝗸𝘂𝘄𝗮𝗸𝗮 𝗺𝗼𝘁𝗼.
Kadri unavyozidi kuongezeka uzito ndivyo unavyozidi kuongeza uzito kwenye pingili zako kama pingili za mgongo, nyayo kuwaka moto, magoti kuuma,

🚨 𝗠𝗼𝘆𝗼 𝗸𝘂𝗽𝗮𝗻𝘂𝗸𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝘀𝗵𝗶𝗻𝗶𝗸𝗶𝘇𝗼 𝗹𝗮 𝗱𝗮𝗺𝘂.
Kadri unavyozidi kunenepa ndivyo moyo wako unavyozidi kusukuma mzigo mkubwa na kupanuka uwezo wa kupata shinikizo la damu kuwa mkubwa kwasababu mwili kungangania maji yasiyokuwa na kazi. ndio mana wenye uzito mkubwa mwili huwa unajaa na kubonyea kama kiazi.

🚨 𝗠𝗮𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝗺𝗰𝗵𝗮𝗿𝘂𝗸𝗼 𝘄𝗮 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶.
Uzito mkubwa unasababisha magonjwa ya aleji kama, pumu ya kifua, pumu ya ngozi na mafua makali. Mwili wa binadamu huwa na kiwango chake cha kuhifadhii mafuta ya ziada kwahiyo endapo mafuta ya ziada yakizidi kiwango kinachotakiwa kwasababu ya uzito mkubwa mtu atapata aleji au mzio sugu.

abstract virus blood cells 1048 12007 600x600

🚨 𝗠𝗮𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝘂𝗴𝘂𝗺𝗯𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗮𝘂𝗺e.
Mwanaume anahomoni ya kiume ambayo inatawala mwilini inayofanya mwanaume kuwa na nguvu, maumbile ya kiume na kufanya apate hamu ya tendo la ndoa. Uzito mkubwa husababisha homoni za kiume zisiweze kutawala mwilini na kufanya ubora wa mbegu za kiume na wingi wa mbegu za kiume kupugua pamoja na hisia za tendo la ndoa kushuka.

🚨 𝗨𝗴𝘂𝗺𝗯𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗺𝘄𝗮𝗻𝗮𝗺𝗸𝗲
Mwanamke anaweza kuoata hitilafu ambazo zinavuruga homoni za kike na kufanya ovari zisiweze kukomaza mayai kila mwezi hata kama unapata hedhi. Uzito mkubwa unasababisha ovari kushindwa kukomaza mayai na ubora wa mayai kupungua na kufanya mwanamke kupata ugumba.

🚨 𝗞𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝘂𝗰𝗵𝗼𝘃𝘂 𝘄𝗮 𝗸𝘂𝘂𝗱𝗺𝘂
Kuna watu wengi tu hawawezi kufanya kazi mbalimbali hata kushindwa kufurahia tendo la ndoa kwasababu ya kuwa na uchovu wa kudumu kwasababu ya uzito mkubwa.

portrait stressed black man 53876 20512 600x400

🚨 𝗦𝗲𝗹𝗶 𝘇𝗮 𝗺𝗶𝘄𝗶𝗹𝗶 𝗸𝘂𝗰𝗵𝗮𝗸𝗮𝗮.
Uzito mkubwa unaweza kusababisha seli za mwili kuchakaa hasa sseli zinazoratibu matumizi ya sukari mwilini na kufanya mtu kuwa katika hatua za awali za kuugua ugonjwa wa kisukari.

🚨 𝗞𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗴𝗲𝘀𝗶, 𝗸𝗶𝘂𝗻𝗴𝘂𝗹𝗶𝗮 𝗮𝘂 𝘁𝘂𝗺𝗯𝗼 𝗸𝘄𝗮𝗸𝗮 𝗺𝗼𝘁𝗼.
Uzito mkubwa husababisha gesi na kiungulia na njaa za mara kwa mara. Ili kuondoa matatizo hayo basi anza kupunguza uzito na utapata matokeo mazuri ndaniya muda mfupi.

Nakushauri usiendelee kukaa na mafuta ya ziada katika mwili wako, anza kuondoa mafuta ya ziada kwa kupunguza uzito ili uepukane na madhara yote ya uzito mkubwa ili kupunguza matatizo ya dawa.

Jifunze zaidi; Tazama Video hii

𝐍𝐁📗📗:
Nakushauri kupata Kitabu cha 𝗦𝗮𝘆𝗮𝗻𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗠𝗮𝗽𝗶𝘀𝗵𝗶 kinatoa elimu ya manunuzi, elimu ya magonjwa ya lishe, elimu ya vyakula sahihi kwa afya na mpangilio wa chakula ili kudhibiti kitambi na uzito mkub.

KWA USHAURI NA MATIBABU
📍Karibu 𝗡𝘀𝗮𝗺𝗯𝗼 𝗛𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵𝗰𝗮𝗿𝗲 tupo mkabala na 𝗵𝗼𝘀𝗽𝗶𝘁𝗮𝗹𝗶 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝘆𝗮𝗺𝗮𝗹𝗮.

Related Articles

Responses

Your email address will not be published. Required fields are marked *